Bundesliga imeanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa tarehe 18 kwa pambano kati ya mabingwa watetezi Bayern Munich na Bayer Leverkusen katika uwanja wa Allianz Arena. Lakini nini kinachotarajiwa mara hii katika msimu huu wa 55 wa Bundesliga, ambapo timu zinazoonekana kuwa na utamaduni wa kushika nafasi za juu kama Schalke 04, Bayer Leverkusen , Borussia Moenchengladbach zimeporomoka na hata hazimo katika mashindano ya ligi ya Europa, mara hii.
Kwa upande wa tetesi za kuhama wachezaji , tetesi kumhusu Ousmane Dembele wa Borussia Dortmund hazija muacha salama. Kila siku tetsi hizo zinazidi kuongezeka akihusishwa na kuhamia FC Barcelona ya Uhispania. Dembele kutokana na utovu wa nidhamu ambapo alishindwa kufika katika mazowezi ya timu hiyo siku ya Alhamis ameadhibiwa kwa kuondolewa katika kikosi cha kwanza na atakaa nje ya kikosi hicho hadi mwishoni mwa mwezi huu.
Dembele amefanya hivyo akitaka kutoa mbinyo kwa timu yake kumruhusu kwenda kuchezea Barcelona. Barcelona wametoa kiasi cha euro milioni 90 pamoja na malipo mengine ya bonasi hapo baadae kuweza kumpata mchezaji huyo chipukizi mwenye umri wa miaka 20, raia wa Ufaransa. Lakini Dortmund wamekataa wakitaka kitita cha euro milioni 140 hadi 150 ili kuweza kumuachia mchezaji huyo.
Barcelona yatakiwa kusajili wachezaji wapya
Barcelona inalazimika kusajili wachezaji wapya , amesema mchezaji wa kiungo wa timu hiyo Sergio Busquets , na timu hiyo inawania kuwasajili Ousmane Dembele wa Borussia Dortmund na Philippe Coutinho wa Liverpool ili kuimarisha kikosi chake kilichoondokewa na mchezaji nyota Neymar ambaye ametimkia Paris St. Germain kwa kitita cha milioni 222.



No comments
Post a Comment