BI. TERACK: MARUFUKU KULIMA KARIBU NA BWAWA LA NYIHOGO-KAHAMA.


Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imetoa Maagizo kwa  Mamlaka ya maji na Mazingira wilayani KAHAMA (KUWASA), kuhakikisha inazuia shughuli za Kilimo katika bwawa la Nyihogo ambalo ni maalum kwa huduma ya maji kwa wananchi wa wilaya  hiyo.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa Bodi  mpya ya KUWASA, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi Zainab Tellack amemtaka mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu kushirikiana na Kuwasa kuwaelimisha wananchi ili wasiendelee na Shughuli za kilimo kwenye eneo la Bwawa hilo.




Amesema Kilimo kinachoendelea katika bwawa hilo kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa binadamu hivyo wananchi   wa eneo hilo waelimishwe kutafuta maeneo mengine ya kufanya shughuli za Kilimo.

Bi Tellack pia ameitaka KUWASA na Bodi yake kuhakikisha inafanya kazi kwa malengo na kwamba miradi yote wanayoanzisha ikamilike kabla ya kuanzisha mingine mipya.
TAG